Yanga imelenga kufanya vizuri katika michuano ya Kimataifa, ndio maana imesajili wachezaji ambao wana uzoefu mkubwa na michuano hiyo
Walianza na Lazarus Kambole ambaye amewahi kuwa mfungaji bora ligi ya mabingwa barani Afrika, wakatua kwa Bernard Morrison ambaye msimu uliomalizika ni yeye aliyewabeba Simba katika michuano ya kombe la Shirikisho
Juzi Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akamtambulisha kiungo Gael Bigirimana, mchezaji mwenye wasifu mkubwa kuliko mchezaji yeyote katika wale wanaocheza soka hapa nchini
Bigirimana alizaliwa October 22 Mwaka 1993 Bujumbura nchini burundi. Ana umri wa miaka 28. Kimo chake ni 1.7m
Bigirimana naweza kuyamudu maeneo mawili uwanjani, kiungo mkabaji na kiungo wa kati.
Bigirimana, amewahi kupitia vilabu kadhaa, mongoni mwao ni Coventry City, Newcastle United, Rangers na klabu ya Grentoran football yenye maskani yake huko Ireland kaskazini.
Mwaka 2013 aliwahi kuichezea timu ya taifa ya ya vijana U20 ya England, alicheza mechi mbili. Kwa sasa analitumikia timu ya taifa ya Burundi
Bigirimana ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia klabu ya Coventry City kutwaa taji la EFL msimu wa 2016- 2017, huku yeye binafsi akitwaa tuzo ya Championship Apprentice of the year award
Bigirimana amecheza jumla ya mechi 258, amefunga magoli 16, assist 21, kadi za njano 44 na nyekundu moja
Ujio wake unamaanisha kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anaweza kumbadilisha majukumu mchezaji bora wa ligi kuu msimu wa 2021/22 Yannick Bangala kwa kumrejesha katika safu ya ulinzi
Yanga imezidi kuimarika zaidi katika eneo la kiungo kwani Bigirimana anaungana na akina Khalid Aucho, Feisal Salum, Salum Abubakar, Zawadi Mauya, Bangala na yule anayetokea Afrika Magharibi ambaye anasubiri kutambulishwa