Uongozi wa Yanga unakusudia kuwaaga kwa heshima baadhi ya wachezaji waliomaliza mikataba lakini hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano Yanga Injinia Hersi Said amesema wamefanya kikao na wachezaji hao na wataachana nao kwa heshima
"Ni kweli kuna wachezaji wamemaliza mikataba lakini wengine hatutakuwa nao msimu ujao. Tunaandaa utaratibu mzuri wa kuwaaga kwa heshima, tunatahamini mchango wao katika klabu ya Yanga," alisema Hersi
Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika na huenda wasiwe sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao ni pamoja na Deus Kaseke, Ramadhani Kabwili, Yassin Mustafa na Paulo Godfrey 'Boxer'
Boxer ameshajiunga na klabu ya Singida Big Stars ambayo pia huenda ikamsajili Deus Kaseke