Ligi kuu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 inaanza kuchezwa leo katika dimba la Azam. Complex Chamazi jijini Dar es salaam
Leo kutakuwa na mechi nne ambazo zote zitaonyeshwa mbashara na Azam TV, zikianza kupigwa kuanzia saa nane mchana
Yanga U20 ambayo ilifika fainali mwaka jana, itaanza kampeni ya michuano hiyo Jumatano kwa kuumana na Geita Gold katika mchezo ambao utapigwa saa mbili na nusu usiku
Msimu huu Yanga U20 imepania kutwaa taji hilo, wakiingia katika michuano hiyo wakiwa na timu iliyoandaliwa sawasawa
Kocha Mwinyi Zahera ndiye Mkurugenzi wa soka la Vijana, akishiriki kikamilifu katika maboresho ya timu hiyo
Benchi la ufundi linaongozwa na Said Maulid 'SMG' akisaidiwa na Fredy Mbuna wakati mkufunzi wa makipa ni Razak Siwa

ADVERTISE HERE