Kikosi cha Yanga kitaondoka Kilimanjaro majira ya saa 10 jioni kurejea Dar es salaam na taji la FA walilotwaa jana baada ya kuichapa Coastal Union kwa mikwaju ya penati 4-1 baada ya matokeo ya sare ya mabao 3-3
Mashabiki wa Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Kaunda, Jangwani kuwalaki mashajaa wao wakirejea na taji la tatu msimu huu
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema leo hakutakuwa na paredi kama walivyofanya wiki iliyopita
Timu itakapotua JNIA itapanda basi la klabu na moja kwa moja kuelekea Jangwani ambako watakabidhi taji la FA kwa Wazee
Shamrashamra zote zitafanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam
ADVERTISE HERE