Yanga iko kamili kuikabili Njombe Mji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2018
Yanga iko kamili kuikabili Njombe Mji
Kikosi cha Yanga kinashuka kwenye uwanja wa Taifa leo kuikabili Njombe katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 17.

Huo ni mchezo wa pili tangu kuanza kwa duru la pili.

Kuelekea mchezo huo kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mkoani Njombe, mYanga ilipata lipata ushindi wa bao 1-0.

Nsajigwa amesema kuwa huu ni wakati wa lala salama na kilichoko katika mipango yao ni kushinda kila mchezo.

Nsajisgwa amesema kama Yanga itashinda mechi zake zote zilizosalia zikiwamo dhidi ya vinara Simba na Azam FC, anaamini nafasi ya kutetea ubingwa ipo.

"Wachezaji wetu wanafahamu ugumu na ushindani uliopo katika ligi, tunawakumbusha kupambana katika dakika zote 90 kwa sababu tunaamini hakuna mechi nyepesi, kuhusu majeruhi, tunajua tutakavyoipanga timu na kila mchezaji aliyesajiliwa ana uwezo wa kuitumikia Yanga," alisema kocha huyo.

Baada ya mechi ya leo, Yanga itaendelea na maandalizi ya kuwakabili St Louise kutoka Shelisheli katika mchezo wa raundi ya awali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’