Jana Asec Mimosas walimuaga kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki baada ya mchezo wa kumaliza msimu wa 2021-22 wa Ligi Kuu Ivory Coast
Aziz Ki alitarajiwa kuondoka Ivory Coast kuja Tanzania jana usiku na huenda akaelekea Arusha kushuhudia mchezo wa fainali kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid kesho Jumamosi
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amethibitisha ujio wa Azaz Ki ambaye baada ya taratibu zote kukamilika, atatambulishwa
Baada ya utambulisho wa mshambuliaji Lazarus Kambole, utambulisho wa Aziz Ki ndio utakaofuatia
ADVERTISE HERE