Yanga imekamilisha msimu wa ligi kuu 2021/22 pasipo kupoteza mchezo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa kuhitimisha msimu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Bao la Denis Nkane lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo muhimu ambao umewafanya wafikishe alama 74
Ni rekodi mpya ya Yanga kumaliza msimu pasipo kupoteza mchezo
Matokeo ya michezo mingine, Biashara United imeungana na Mbeya Kwanza kushuka daraja baada ya kuchapwa mabao 4-1 na Azam Fc
Tanzania Prisons imechapwa na Ruvu Shooting bao 1-0, imeungana na Mtibwa Sugar kucheza play-off
George Mpole wa Geita Gold ameibuka mfungaji bora na mabao 17
Mpole alifunga bao pekee la Geita Gold katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mayele alifunga bao kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye dakika za majeruhi lakini mwamuzi alikataa bao hilo kwa kudhani Mayele alikuwa ameotea
