Yanga ilivyoipelekea 'Neema' Lipuli FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
5 Feb 2018
Yanga ilivyoipelekea 'Neema' Lipuli FC
Licha ya kipigo, lakini klabu ya Lipuli FC imenufaika na ujio wa Yanga mjini Iringa baada ya kuvuna kiasi cha Sh18 milioni kutokana na mgao wa mapato ya pambano lao la Ligi Kuu Bara lililopigwa juzi Jumamosi ambapo liliingiza Sh 58.4 milioni.

Kiwango hicho cha fedha ni rekodi kwa Uwanja wa Samora, kwani haijawahi kutokea pambano lolote, sio la msimu huu tu bali hata mechi za nyuma kuingiza kiasi kama hicho cha fedha.

Yanga ilioibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo huo, iliambulia Sh 9 milioni na msimamizi wa kituo hicho, Elias Mwanjala alisema katika makusanyo hayo mbali na fedha zilizopata Lipuli na Yanga fedha nyingine zilipelekwa kwenye maeneo mengine kama gharama za mchezo, kodi, TFF na Bodi ya Ligi.

“Hii imevunja rekodi katika Uwanja wa Samora kwani umeingiza Sh 58.4 milioni, haijawahi tokea kabisa na katika mchezo ule hakuna hata tiketi moja iliyobainika kuchachukuliwa. Kulikuwa na usimamizi mzuri sana kwenye suala la tiketi,” alisema.

Mwanjala alisema katika makisio yao ilikuwa waingizie mashabiki 10,000 uwanjani lakini hali ilikuwa tofauti, watu walizidi mara madufu.

Akizungumzia hatua ya timu zote mbili kugoma kuingilia geti kuu na badala yake kuamua kutumia geti dogo linalotumiwa na viongozi, Mwanjala alisema timu zote zilivunja kanuni za mpira na adhabu yake ni kupigwa faini.

“Unajua klabu hizi zinaamini katika ushirikina, kitu ambacho TFF hatuamini katika jambo hilo, hivyo wanaona bora walipe faini na hata suala la wachezaji kutoingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo ni kosa ambalo pia linastahiki kupigwa faini, kwa kuwa ni kosa kufanya hivyo.”

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
51m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →