Baada ya shamra shamra za kihistoria ambazo Wananchi wameshangilia ubingwa wao wa 28 hapo jana, bado kazi haijamalizika msimu huu
Tayari ubingwa umeingia katika makabati ya Yanga pale Jangwani lakini Wananchi wamedhamiria kumaliza msimu pasipo kupoteza mchezo
Ligi inafika tamati keshokutwa Jumatano, Yanga ikimalizia mchezo wa mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni dakika tisini muhimu kwa Wananchi kuhakikisha hawapotezi mchezo huo ili kunogesha ubingwa kwa kumaliza msimu pasipo kupoteza mchezo
Mtibwa Sugar wao wanahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea kubaki ligi kuu msimu ujao
Jana Mtibwa Sugar walichapwa mabao 4-2 na Namungo Fc katika uwanja wao wa Manungu na hivyo kujiweka katika hatari ya kucheza playoff ya kubaki ligi kuu
Baada ya mchezo huo Julai 02 Yanga itakamilisha msimu kwa mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Coastal Union mkoani Arusha