Kikosi cha Yanga kinaondoka mkoani Mbeya asubuhi ambapo majira ya saa tano asubuhi kitatua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Shamrashamra za ubingwa zitaanza uwanja wa Ndege ambapo Yanga imebainisha barabara ambazo basi maalum litakalobeba wachezaji litapita kuelekea Makao Makuu ya klabu Jangwani
Leo ni siku ya Wananchi, shughuli zitasimama kwa muda katika jiji la Dar es salaam kupisha shamrashamra za ubingwa wa 28 wa Yanga!


ADVERTISE HERE