Tukio alilofanyiwa Okwi si la kimichezo

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
5 Feb 2018
Tukio alilofanyiwa Okwi si la kimichezo
Jana mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi alipigwa ngumi ya koo na mlinzi wa Ruvu Shooting Mau Bofo ambaye naye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Okwi alipoteza fahamu kwa dakika kadhaa kabla madaktari wa Simba hawajawahi kuokoa maisha yake.

Lile halikuwa tukio la kimchezo kabisa kwani lilihatarisha maisha ya mchezaji.

Kwa mchezaji ni muhimu kuzuia mihemko, bila hivyo unaweza kujikuta unafanya tukio linaloweza kuigharimu timu yako.

Wachezaji wanafundishwa mbinu mbalimbali za kutafuta ushindi ikiwemo ya kuwatafutia kadi kwa makusudi wachezaji wa timu pinzani sasa usipokuwa makini unajikuta unaingia katika mtego

Kutolewa kwa Bofu mapema kuliondoa zaidi mchezoni Ruvu Shooting na bila shaka anasubiri adhabu kubwa zaidi ya kufungiwa.

Kwa mashabiki wenzangu wa Yanga nawaasa ushabiki wetu usivuke mipaka.

Si vizuri kufurahia tukio lililompata Okwi, lile lilikuwa sio tukio la kimchezo, tukio la hatari sana.

Nakumbuka taharuki kama ile ilimpata mchezaji wetu Emanuel Martin Songea alipopigwa kiwiko na Juma Salamba wa Majimaji, ambapo alipoteza fahamu na kupelekea akimbizwe Hospitalini kuokoa maisha yake.

Bahati mbaya tukio lile mwamuzi wa mchezo hakuliona lakini Kamati ya Masaa 72 iliweza kulibaini na mchezaji yule kufungiwa.

Kwa wenzetu Ulaya hawaungi kabisa mkono matukio ya aina hii, achilia mbali kufungiwa kwa muda mrefu kwa mchezaji, unaweza kujikuta unatimuliwa kabisa na timu yako.

Hapa kwetu Tanzania, ni juzi tu Singida United ilionyesha mfano walipomfungia kwa muda usiojulikana mchezaji wao wa Kimataifa Papi Kambale, aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Green Worriors baada ya kufanya madhambi ya makusudi.

Nakumbuka mwishoni mwa mwaka jana, nchini Ufaransa, Patrice Evra alitimuliwa na Marseille baada ya kumpiga teke shabiki wa timu pinzani wakati timu yake ikipasha kujiandaa na mchezo.

Mchezaji kama Luis Suarez amekumbana na matukio mengi ya kufungiwa kwa muda mrefu kutokana na utovu wa nidhamu ingawa sasa amejifunza na kuwa 'mtoto mwema.'
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’