Mabingwa wa ligi kuu ya NBC Yanga jioni ya leo wanashuka katika uwanja wa Sokoine kuikabili Mbeya City
Baada ya mchezo huo Yanga itakabidhiwa rasmi ubingwa katika hafla itakayojiri katika dimba la Sokoine
Yanga imefanikiwa kuurejesha ubingwa Jangwani baada ya kuupoteza katika misimu minne iliyopita
Baada ya Yanga kukabidhiwa kombe, shamrashamra zitaanzia hapo Mbeya na kuendelea jijini Dar es salaam kesho Jumapili Yanga
Kuna mfululizo wa matukio ambayo Yanga imeyaandaa msemaji wa timu hiyo Haji Manara akitamba kuwa wanakwenda kuwafundisha wengine vile wanapaswa kufanya katika kusherehekea ubingwa
Basi maalum ambalo litatumika kuwabeba wachezaji jijini Dar es salaam tayari limewasili Manara akibainisha kuwa leo watakamilisha 'branding' ya basi hilo