Mshambuliaji Chico Ushindi jana aliendeleza pale alipoishia kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union akipachika bao lake la pili kwenye ligi msimu huu
Chico alianza maisha yake na Yanga kwa kusuasua akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyotishia hatma yake
Chico sasa amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao (katika mashindano yote)
Yanga inatarajiwa kusajili nyota wanne wa kigeni na italazimika kuacha mchezaji mmoja ili kuwa na wachezaji 12 kukidhi kanuni za usajili wa ndani
Baada ya kumshuhudia katika michezo miwili mfululizo akicheza kwa takribani dakika 120, bado kuna wenye mashaka nae?
Benchi la ufundi lina mtihani wa kuamua mchezaji wa kuacha ingawa tetesi zilizopo ni kuwa mshambuliaji Heritier Makambo anaweza kujiunga na Singida Big Stars (zamani DTB)