Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ubora wa mlinzi wa kati Ibrahim Bacca umempa matumaini ya kuendelea kuwa na safu bora ya ulinzi katika msimu ujao
Bacca aliyesajiliwa na Yanga dirisha dogo akitokea KMKM, jana kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, aliitumika kwa dakika 90 kwa mara ya kwanza na kuonyesha kiwango bora
Nabi amesema walifanya 'scouting' nzuri kumnasa mlinzi huyo na kuondoa ulazima wa kutumia gharama kubwa kusaka beki nje ya nchi
"Ni beki mzuri ambaye hata katika viwanja vya mazoezi anafanya vizuri. Tumeona ni wakati sahihi kumpatia nafasi ili aweze kuzoea mazingira. Nadhani ametupa imani na kutofikiria kwenda nje ya nchi kusaka beki mwingine," alisema Nabi
Bacca anawakumbusha Wananchi nahodha wao wa zamani Nadir Haroub 'Cannavaro'