Keshokutwa Jumatano Yanga itacheza mechi ya mwisho nyumbani msimu huu dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka mashabiki wao kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo wa kuhitimisha msimu kwa michezo ya nyumbani
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea mkoani Mbeya ambako wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Mbeya City
Wananchi watakabidhiwa ubingwa mkoani Mbeya na kurejea nao jijini Dar es salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Arusha ambako watacheza na Mtibwa Sugar Juni 29
Yanga imeupeleka mchezo dhidi ya Mtibwa mkoani Arusha dimba la Sheikh Amri Abeid ili wapate muda mzuri wa maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Julai 02 katika uwanja huo wa Sheikh Amri Abeid