Jana mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele alishiriki kwenye mchezo wa hisani maarufu Nifuate akiwa katika timu ya Ali Kiba wakipambana na timu ya Mbwana Samatta
Mayele alicheza katika kikosi cha Kiba sambamba na mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Wydad Athletic Saimon Msuva ambaye katika mchezo huo alipachika mabao mawili
Pamoja na kuwa Mayele hakufunga katika mchezo huo, wengi walivutiwa na jinsi alivyokuwa akishirikiana na Msuva katika safu ya ushambuliaji ambayo iliongozwa na Ali Kiba
Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya wapi Msuva ataelekea, mwenyewe amesema siku sio nyingi ataweka wazi hatma yake
Wakati Yanga ikitangaza ubingwa kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, Msuva alikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo
Akihojiwa baada ya mchezo, Msuva alikiri kuwania na klabu zote kubwa hapa nchini lakini akabainisha kuwa siku chache zijazo hatma yake itafahamika
Yanga ina nafasi nzuri zaidi ya kumnasa Msuva kama ataamua kubaki nchini ingawa inaelezwa kuwa ana ofa nyingi nje ya nchi pia