Kampeni ya Nani Zaidi imebadilishwa jina na kuitwa Klabu Yangu ikiihusisha klabu ya Simba pekee baada ya Yanga kujitoa
Kampeni hiyo ilianzishwa na Azam Media wakizishindanisha Yanga na Simba kwa mashabiki wao kupiga kura kwa tuchangia Tsh 1,000/- kwa kila kura
Akizungumza na Wanahabari juzi, Msemaji wa Yanga Haji Manara alithibitisha Yanga kujitoa kwenye kampeni hiyo huku akibainisha kuwa watatoa taarifa rasmi kuhusu uamuzi huo
Moja ya sababu inayotajwa kupelekea Yanga kujitoa ni kutokana na kuwa na miradi mingine ambayo inawahitaji mashabiki wao kushiriki kwa kutoa fedha
Yanga inaendelea na mradi wa kuandikisha Wananchama pamoja na kutoa kadi ambapo gharama ya kuwa Mwanachama ni Tsh 31,000
Hivi karibuni Yanga itaanza kuandikisha mashabiki na kuwapa kadi za mashabiki gharama itakuwa Tsh 17,000/-
Yanga imeamua kujikita zaidi katika miradi hii ambayo ni muhimu zaidi kwa maslahi ya klabu na Wanachama wao