Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama klabu ya Yanga Simon Patrick amesema wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Lazaros Kambole kwa kufuata mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi
"Lazarous Kambole ndiyo mchezaji anayeshikilia rekodi ya hatrick ya haraka zaidi kwenye mashindano ya CAF champions league (dakika 5). Kocha Nabi kahitaji huduma yake na sisi Wananchi tukamletea hitaji lake, muda utaongea," aliandika Simon kwenye ukurasa wa mtandao wa jamii
Kambole amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akitokea klabu ya Kaizer Chiefs

ADVERTISE HERE