Kikosi cha Yanga leo majira ya saa mbili na nusu usiku watashuka kunako uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili wagosi wa Kaya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC raundi ya 27
Ni katka mchezo huo Yanga wanaweza kutwaa ubingwa kama wataibuka na ushindi
Kwa hakika umekuwa msimu bora sana kwa Yanga ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote
Ushindi kwa Yanga leo utakuwa na maana kubwa kwa Wananchi kwani watamaliza ukame wa kukosa taji la ligi kuu kwa msimu minne
Lakini pia utakuwa ushindi wa heshima kwa wadhamini GSM ambao wamegharamia usajili katika misimu miwili iliyopita
Wakati Yanga wanafanya usajili yalisikika maneno ya kubeza kuwa 'wanasajili wacongo wengi kama wanafungua bendi ya muziki'
Hata pale msimu ulipoanza na Yanga kushinda michezo mitano ya kwanza, bado kejeli zilisikika kuwa ni 'timu ya dakika 45 tu kipindi cha pili wanakata moto'
Ikafika wakati wakabaki na ile kauli wanayoitumia kila msimu 'Ni kawaida yao kuongoza ligi lakini mwishoni Simba wanachukua ubingwa'
Kuna wakati wakawa wanataja mechi ambazo waliamini Yanga ingefungwa lakini jambo hilo halikutokea, zaidi wanakwenda kutwaa ubingwa wakiweka rekodi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa karibu msimu mzima
Ni msimu ambao watani zao Simba hawajaonja radha ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi japo hata kwa sekunde moja tu!