Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na kiungo Feisal Salum wameibua shangwe kwa wabunge mara baada ya Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Mwigulu Nchemba kutaja majina yao.
Shangwe hilo limetokea jana Juni 14, 2022 bungeni wakati Mwigulu akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka 2022-2023.
Mara baada ya Mwigulu kutaja majina ya wachezaji hao wabunge walianza kushangilia kwa kupiga makofi.
"Nampongeza GSM kwa kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa usajili wa Fiston Mayele. Mayele amekuwa maarufu kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa" Waziri Mwigulu alisema
Dk Mwigulu pia aliweka utani kwa kumuomba radhi Waziri Mkuu kwa bao la Fei Toto alilowafunga Simba kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA jijini Mwanza
"Nachukua fursa hii kuwapongeza Yanga kwa mwenendo wao mzuri sana mwaka huu na nitumie fursa hii kumuomba radhi bosi wangu Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kitendo alichowafanyia mwanangu Fei Toto kule Mwanza
"Mniwie radhi nilipompeleka Fei Toto Yanga sikujua atakuja kuwafanyia kitu mbaya hivi, mpaka nasikia anatafutwa maliasili eti kaua mnyama bila kibali"