Mpaka sasa Yanga ina nafasi tatu za wachezaji wa kigeni ambazo hakuna shaka watazijaza katika dirisha la usajili ambalo litafunguliwa mwishoni mwa mwezi huu
Yanga ilikuwa na wachezaji 10 wa kigeni kabla ya kuachana na Saido Ntibazonkiza ambaye mkataba wake umemalizika, sasa wamebaki na wachezaji tisa
Djigui Diarra, Djuma Shabani, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Fiston Mayele, Yacouba Songne, Heritier Makambo na Chico Ushindi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Yanga Haji Manara jana kuwa mabingwa hao watarajiwa wa ligi kuu ya NBC wataongeza wachezaji wanne
Ni wazi kuna mchezaji mmoja ambaye Yanga italazimika kumuacha ili kubaki na wachezaji 12
Mkataba wa Yacouba Songne unamalizika mwishoni mwa msimu huku ikielezwa kuwa winga Chico Ushindi awali alipewa mkataba wa miezi sita kukiwa na makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili kama Yanga itaridhishwa na kiwango chake