Kikosi cha Yanga leo kinaingia kambini kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa Jumatano, Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanaingia kambini wakiwa na wachezaji wote
"Timu inatarajiwa kuingia kambini leo tukiwa na wachezaji wote. Tuliwapa mapumziko ya siku mbili wachezaji waliokuwa kwenye timu za Taifa, tunafurahia wote wamerejea na taarifa ya daktari wa timu inaonyesha hakuna mchezaji aliyepata majeraha katika timu za Taifa"
"Hii ni wiki muhimu sana kwetu, tunahitaji kushinda mchezo dhidi ya Coastal Union ili tuweze kuwa mabingwa," alisema Bumbuli
Mchezo huo wa 'kukata na shoka', utapigwa kuanzia saa mbili na nusu usiku