Kocha wa zamani wa Kagera Sugar ambaye sasa anawanoa vijana katika Academy ya Cambiasso, Mecky Maxime amesema kiungo wa Yanga Yannick Bangala anastahili kuwa mchezaji bora wa ligi kuu msimu huu
Mexime amesema kwa mtazamo wake Bangala ndiye mchezaji bora katika kikosi cha Yanga msimu huu lakini pia hakuna mchezaji mwingine katika ligi anayeweza kumfikia
"Niseme wazi kwangu katika kikosi cha Yanga na hata waliopo katika Ligi Kuu Bara, Bangala ndiye mchezaji bora. Huu ni mtazamo wangu tu, lakini natambua wanaoshughulika na kazi ya kuchagua mchezaji bora wanajua zaidi," amesema Maxime
Bangala amekuwa na kiwango bora katika kikosi cha Yanga akitumika kama mchezaji kiraka katika safu ya ulinzi na kiungo
Nyota huyo kutoka Congo DR, amethibitisha ubora wake kila wakati alipoingia dimbani kuitumikia Yanga