Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela leo ametangaza kumuunga mkono Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said anayewania Urais wa klabu ya Yanga
Hersi amerudisha fomu leo, zikirudishwa na Mzee Mohammed Msumi kwa niaba yake
Akizungumza katika tukio hilo lililofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mwakalebela alitangaza kuwa hatagombea katika uchaguzi ujao lakini atamuunga mkono Hersi
"Mimi nimekuja hapa kwa mambo mawili, moja ni kuwatangazia Wapenzi na Wanachama wa Yanga kuwa sitagombea katika uchaguzi ujao, pili natangaza kumuunga mkono Injinia Hersi Said anayewania nafasi ya Urais"
"Hivi ni lini uliiona Yanga ikicheza na Hersi akakosekana, ni lini tumeiona Yanga ikitembeza bakuli katika nyakati zote ambazo Hersi yuko nasi?. Kazi kwenu Wanachama lakini nadhani Hersi ndiye mtu sahihi anayefaa kutuongoza," alisema Mwakalebela
Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu linafungwa leo saa 10:30 jioni