Kesho Jumatano, Juni 08 2022, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili vigogo wa soka barani Afrika Algeria katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Afcon 2023
Tanzania inahitaji kushinda mchezo huu ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo. Lengo kuu ni kuhakikisha Tanzania inachukua alama tisa katika michezo yote mitatu itakayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Walinza vyema katika mchezo wa kwanza ugenini wakipata alama moja dhidi ya Niger katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Watanzania wameaswa kujitokeza kwa wingi dimba la Mkapa siku ya kesho kuishangilia timu yao
TFF wametangaza viingilio vya mchezo huo ambapo Mzunguuko ni Tsh 3,000/- wakati VIP A, B na C ni Tsh 5,000/-
