Wiki ijayo Juni 15 2022, kikosi cha Yanga kitashuka dimba la Benjamin Mkapa kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC raundi ya 27
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kwani alama tatu zitawahakikishia Wananchi kutwaa ubingwa msimu huu
Wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wanaendelea na mazoezi makali Avic Town kujiandaa na mchezo huo


Yanga inakabiliwa na michezo miwili muhimu dhidi ya Coastal Union ambayo inaweza kuwapa ubingwa
Baada ya mchezo wa Juni 15, timu hizo zitakutana tena kwenye mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Julai 02
ADVERTISE HERE