Ushindi ni lazima kwa Yanga leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
3 Feb 2018
Ushindi ni lazima kwa Yanga leo
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amesema kama Yanga itashindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Lipuli ya Iringa itakuwa imejiweka pabaya katika kuutetea ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Lwandamina, amesema kuwa kwenye mchezo wa leo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, wana kila sababu za kuhakikisha wanapata ushindi ili kuendelea kuifukuzia Simba inayoongoza ligi.

Yanga itaingia kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18 tangu Lipuli ilishuka daraja mwaka 1999 na kuwafanya mashabiki wa mkoa wa Iringa kushindwa kuziona timu kubwa na kongwe zenye mashabiki wengi, ikiwemo Yanga.

“Ni mchezo mgumu kama ilivyo michezo mingine, tupo ugenini lakini kwa namna mambo yalivyo ni lazima tupambane ili kutoongeza pengo la pointi na wanaoongoza ligi,” alisema Lwandamina.

Yanga imeachwa kwa pointi saba na Simba wenye pointi 35 huku Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiachwa kwa pointi tano na vinara hao, kikosi cha Lwandamina kinashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 28.

Nae nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’, amesema watahakikisha wanapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha wanapata ushindi.

“Tulitoka sare kwenye mchezo wetu wa kwanza Dar es Salaam, hiyo inaonyesha Lipuli si timu ya kuibeza, kama wachezaji tutahakikisha tunakuwa makini na kupambana muda wote,” alisema Canavaro.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →