Jana historia iliandikwa kwa timu ya Taifa ya Wanawake umri chini ya miaka 17 kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya Cameroon
Serengeti Girls imejihakikishia kuwa miongoni mwa mataifa 17 yatakayoshiriki michuano hiyo nchini India
Ni historia kwa sababu hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupata nafasi ya kushiriki kombe la Dunia kwa soka la Wanawake
Mafanikio Haya yawe chachu kwa kaka zao kupambana ili wakati mwingine nao waweze kufikia hatua hii
Hongera Serengeti Girls kwa heshima hii mlioileta Tanzania
ADVERTISE HERE