Kuelekea uchaguzi wa Yanga ambao unapaswa kufanyika Julai 10, mambo muhimu ambayo Mwanachama wa Yanga unapaswa kuyafahamu;
1. Nafasi zinazoshindaniwa ni saba (7), ambazo ni Rais, Makamu Rais na Wajumbe watano (5).
2. Fomu zinapatikana Makao Makuu ya Klabu Jangwani kwa ada ya Tsh. 200,000/= kwa nafasi ya Rais na Makamu Rais, na Tsh. 100,000/= kwa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
3. Malipo yote yafanyike Benki kupitia akaunti ya Klabu, na pindi mgombea anapokuja kuchukua fomu anakuja na risiti ya Benki ya malipo kwa nafasi anayogombea ndipo atapewa fomu.
4. Mgombea anapokuja kuchukua fomu lazima aje na Kadi ya Uanachama au kama bado hajapata kadi aje na ujumbe wa kulipia ada uliotumwa kwenye simu yake baada ya kulipia ada.
5. Fomu zitatolewa na kurejeshwa muda wa kazi kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni (Jumatatu - Ijumaa).