Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo saa moja usiku kitashuka uwanjani kule Benin kuikabili Niger katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023
Ni michezo ya raundi ya kwanza kundi F ambalo linaundwa na Tanzania, Algeria, Niger na Uganda
Tanzania inasaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon kwa mara ya tatu katika historia yake, ni muhimu kupata matokeo mazuri ugenini, kama sio ushindi hata sare
Katika kundi, timu mbili zitakazomaliza kwenye nafasi za juu zitafuzu kwa michuano hiyo
Baada ya mchezo huo Tanzania itarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Juni 08

ADVERTISE HERE