Eneo la ushambuliaji Yanga inahitaji kuongeza mchezaji mwingine ambaye atakuwa na uwezo sawa au zaidi ya Fiston Mayele ambaye msimu huu hakuna shabiki anaweza kuwa na mashaka nae kutokana na kazi nzuri anayofanya uwanjani
Safu ya ulinzi upande wa kushoto ni nafasi nyingine ambayo ni wazi inahitaji kuongezewa nguvu
Uamuzi wa kocha Nasreddine Nabi kumtumia Kibwana Shomari upande wa kushoto ni ishara kuwa walinzi David Bryson na Yassin Mustafa hawajafanikiwa kuingia katika mfumo wake
Tayari Yanga imeachana na Saido Ntibazonkiza ambaye alikuwa na mchango mkubwa msimu huu akifunga mabao saba na kutoa pasi nne za mabao kwenye ligi
Mbadala wake anapaswa kuwa mchezaji ambaye atakuja kufanya zaidi ya vile alivyofanya Saido
Eneo la winga nalo ni wazi linahitaji kuongezewa nguvu. Yacouba Songne anatarajiwa kurejea lakini ni wazi atahitaji muda kuweza kurudisha utimamu wake
Yacouba amekosekana uwanjani tangu mwezi Novemba 2021 baada ya kuumia goti
Usajili wa Yanga uzingatie mahitaji ya michuano ya ligi ya mabingwa zaidi. Baada ya mafanikio makubwa kwenye michuano ya ndani msimu huu, itakuwa aibu kwa Yanga kama itashindwa kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani AfrikaΒ
Itakuwa aibu zaidi kama Yanga itaondoshwa hatua za awali katika michuano hiyo
Na Sele Mchambuzi