Mchakato wa mabadiliko Yanga waiva

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Feb 2018
Mchakato wa mabadiliko Yanga waiva
Kamati ya Mabadiliko iliyoundwa na uongozi wa Yanga mwishoni mwaka 2017 kushauri juu ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga, iko mbioni kumaliza kazi yake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili, Alex Mgongolwa amesema Kamati hiyo inatarajiwa kukutana hivi karibuni kufikia mwafaka juu ya mapendekezo ya mfumo wa uendeshaji ulioridhiwa.

Kamati hiyo inatarajiwa kuwasilisha mapendekezo yake kwa kamati ya utendaji ya Yanga baada ya kukamilisha kazi yake.

Baada ya kamati ya utendaji kukabidhiwa mapendekezo hayo, itaitisha Mkutano Mkuu wa dharura ili wanachama wa klabu ya Yanga waweze kuridhia ama kukataa mfumo huo wa uendeshaji utakaokuwa umependekezwa.

Kukamilika kwa mchakato huo kutaiwezesha Yanga kuanza kuendeshwa kwa mfumo mpya ambao utakuwa ama wa kampuni au hisa kama ilivyo kwa klabu ya Simba.

Kamati hiyo ya Mabadiliko ilikutana mwanzoni mwa wiki hii sasa ikitarajiwa kukutana tena kukamilisha kazi hiyo.

Wanaounda kamati hiyo ni Mwenyekiti Wakili Alex Mgongolwa, wajumbe ni Said Mecky Sadick, Profesa Mgongo Fimbo, Felix Mrema, George Fumbuka na Mohammed Nyengi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’