Yanga yapania kufanya makubwa Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jun 2022
Yanga yapania kufanya makubwa Kimataifa

Uongozi wa klabu ya Yanga, umeelezea mikakati yao kuelekea msimu ujao kuwa ni kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa wanayotarajia kushiriki kutokana na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga inahitaji pointi tatu ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, lakini pia imetinga fainali ya Kombe la FA, endapo itabeba taji hilo itakuwa na nafasi nyingine ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf).

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa klabu hiyo, Hersi Saidi ameeleza kuwa moja ya mikakati yao ni kuzidi kukiboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa wa michuano hiyo, jambo ambalo anaamini litawasaidia kufikia malengo yao.

"Ukweli hiki ambacho wamekiona msimu huu ni kidogo, msimu ujao tumepania kufanya kufuru zaidi kwenye usajili tayari kuna wachezaji tuponao kwenye mazungumzo na wengine wameshasaini mikataba ya awali na uzuri usajili wetu una baraka za wakuu wetu wa benchi la ufundi kwa hiyo mashabiki watulie," alisema Hersi.

Hersi amesema kuwa kwa hatua ambayo Yanga imefikia wachezaji ndio wanalilia kutaka kusajiliwa na siyo wao kumbembeleza mchezaji, lakini hiyo imetokana na mafanikio na ubora ambao timu hiyo imeuonesha msimu huu wa ligi

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’