Kiungo mshambuliaji Farid Mussa ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika lakini tayari makubaliano ya kumuongezea mkataba yamefikiwa, imefahamika
Farid anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia Wananchi mpaka mwaka 2024
Mmoja wa wachezaji walioimarika sana msimu huu, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi akimtumia kama mchezaji kiraka
Kiwango bora kimemrejesha katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' akiwa mmoja wa wachezaji nane wa Yanga walioitwa kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Niger na Algeria
ADVERTISE HERE