Siku moja kabla ya mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba ambao ulipigwa uwanja wa CCM Kirumba juzi na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, viongozi wa Yanga chini ya Udhamini wa GSM, walitembelea na kutoa misaada kituo cha Watoto wenye mahitaji cha SOS Children's Village Mwanza, Mjini
Msimu huu mafanikio ya Yanga hayako uwanjani tu, lakini pia imewapa tabasamu wengi wenye uhitaji kupitia misaada mbalimbali ambayo wameendelea kuitoa katika kila mkoa wanakoenda kucheza
Ni utaratibu wa kipekee ambao unaitofautisha Yanga na klabu nyingine, ndio maana hii ni timu ya WANANCHI







ADVERTISE HERE