Mayele ameacha jina Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2022
Mayele ameacha jina Mwanza

Baada ya kuteka hisia za wapenda soka nchini kutokana na kumuita mwanae jina la nyota wa Yanga, Fiston Mayele, shabiki wa Yanga, Victor Maguta amesema kwa kuwa hana uwezo wa kujenga sanamu la mchezaji huyo nyumbani kwake ameamua kumuita mwanae jina hilo ili kuweka kumbukumbu kwa vizazi juu ya staa huyo.

Maguta (43) ambaye ni mkazi wa Igoma jijini Mwanza na mke wake, Joyce Maguta (30) wameamua kumuita mtoto wao mwenye umri wa miezi minne jina la Fiston Mayele kama ishara ya mapenzi makubwa waliyonayo kwa mchezaji huyo raia wa DR Congo

Maguta amesema Mayele alipojiunga na Yanga mke wake alikuwa na ujauzito wa miezi miwili hivyo kutokana na namna ambavyo Mayele amekuwa akiteka hisia za mashabiki kwa kupachika mabao kama wanandoa walikubaliana kumuita mtoto wao jina hilo.

"Nimetokea kumuita mtoto wangu Mayele kwa sababu pale mwanzoni watoto wangu nilikuwa nawaita majina ya ukoo kwahiyo nikaona huyu wa mwisho niweke mnara wa kwangu kama mpenzi mshabiki wa Yanga watoto wangu watajua kwamba baba yetu alikuwa mshabiki wa Yanga"

"Hata akihama kutoka Yanga siwezi kubadilisha jina la mwanangu hiyo ni kumbukumbu, nilipendezwa tu na uchezaji wa Mayele nikasema kwamba akizaliwa mtoto wa kiume lazima nitamuita Mayele ili nijenge sanamu kwangu kwa sababu sina uwezo wa kujenga sanamu barabarani kwahiyo nikaona nikiita jina itakuwa kumbukumbu kwamba alipita mchezaji wa Yanga ambaye alitikisa kweli," amesema Mguta

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’