Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo aliwafanyia 'suprise' Simba kwa kubadili mfumo wa uchezaji wa kikosi chake
Ni hivi mapema tu Yanga iliachia kikosi 'fake' ambacho kilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema tu lakini ulikuwa ni mkakati maalum
Kwenye mchezo wenyewe Nabi akaingia na kikosi kingine kabisa tena akibadili mfumo uliozoeleka wa 4-2-3-1 kwenda 3-5-2 akiweka viungo wengi katikati ya uwanja
Yanga ilitawala mchezo huo eneo la kati huku Djuma Shabani na Kibwana Shomari wakitumiwa kama walinzi washambuliaji wa pembeni
Yanga leo ingeweza kufunga zaidi ya mabao matatu kama wangetumia vyema nafasi walizotengeneza
Katika michezo miwili ya ligi kuu ambao ilimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, Nabi alitumia mshambuliaji mmoja (Mayele) ikawa rahisi kwa walinzi wa Simba Hennock Inonga na Joash Onyango kumdhibiti
Lakini leo hali ilikuwa tofauti Heritier Makambo na Mayele walianza pamoja, wote wangeweza kufunga kama wangetumia nafasi kadhaa walizopata
Nabi ndiye kocha bora msimu huu, hakuna shaka atakabidhiwa tuzo yake msimu utakapomalizika!