Nani aanze, nani asubiri dhidi ya Simba leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2022
Nani aanze, nani asubiri dhidi ya Simba leo?

Jioni ya leo Wananchi wanashuka uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Simba katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)

Baada ya kambi ya siku nne mkoani Shinyanga, Wananchi wataingia uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo wakiwa na dhamira moja tu, kupata ushindi ili kutinga fainali

Katika kikosi cha Yanga leo atakosekana mkongwe Saido Ntibazonkiza aliyesimamishwa sambamba na Dickson Ambundo kutokana na utovu wa nidhamu

Hata hivyo Yanga inao wachezaji wengine ambao wanaweza kucheza katika nafasi yake pasipo matatizo yoyote

Pengine Chico Ushindi leo anaweza kuanza. Baada ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, Ushindi sasa anaonekana kuwa imara kiafya akicheza kwa takribani dakika 60 katika mchezo uliopita dhidi ya Biashara United

Farid Mussa ni mchezaji mwingine ambaye anaweza kuanza nafasi ya Saido. Ukizungumzia wachezaji ambao wako 'onfire' kwenye kikosi cha Yanga, Farid ni mmoja wao

Bila shaka hakutakuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi, ni utamaduni wa makocha wote duniani kutobadili timu ya ushindi

Ni Djigui Diarra na safu yake ya ulinzi yenye Djuma Shabani, Kibwana Shomari, Dickson Job na Bakari Nondo Mwamnyeto wakati Yannick Bangala anaweza kusogezwa kwenye eneo la kiungo akianza na Khalid Aucho

Jesus Moloko, Ushindi/Farid/Ngushi wanaweza kuanza katika nafasi za winga wakati Feisal Salum na Fiston Mayele wakiongoza safu ya ushambuliaji

Suprise pekee inayoweza kutarajiwa ni kwa Salum Abubakar 'Sure Boy' kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza mabadiliko ambayo yanaweza kumrudisha Bangala kwenye eneo la ulinzi

Sureboy amekuwa na kiwango bora sana akiiongezea Yanga ubora kwenye umiliki wa mpira. Fundi huyu hata kwenye viwanja vyenye changamoto yeye anateleza tu kama yuko 'Anfield'

Wananchi wana historia ya kipekee katika uwanja wa CCM Kirumba kwani katika michezo sita waliyocheza dhidi ya Simba, wameshinda minne, kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’