Wananchi wako jijini Mwanza kuwapa furaha mashabiki wao katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya watani zao Simba
Mchezo huo utapigwa uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa tisa na nusu Alasiri
Unapozungumzia timu bora msimu huu ipo moja tu, ni YANGA. Ndio Wananchi mpaka sasa hawajapoteza mchezo wowote kwenye ligi na michuano ya FA
Wananchi wana nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa ligi kuu wakihitaji alama tatu tu kutoka michezo minne iliyobaki
Lakini sherehe za ubingwa hazitanoga kama itatokea wamepoteza mchezo leo dhidi ya Simba, ndivyo ilivyo!
Hivyo mchezo wa leo una umuhimu mkubwa pengine kuliko mechi zote ambazo wamecheza msimu huu katika mashindano yote
Vijana wa kocha Nasreddine Nabi wamepata maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo wakiweka kambi mkoani Shinyanga
Kilichobaki ni kutumia vyema dakika 90 au 120 katika mchezo wa leo kupata ushindi ambao utawapeleka fainali
Hata hivyo ni dabi, wachezaji watapaswa kupambana kwa muda wote wa mchezo kwani michezo ya dabi wakati mwingine imekuwa haitabiriki
Nyota wawili Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo hawatakuwa sehemu ya mchezo huo baada ya kusimamishwa kutokana na makosa ya utovu wanidhamu
Mshambuliaji Yacouba Songne nae hatarajiwi kuwa sehemu ya mchezo huo akiendelea na program maalum kabla ya kurejea kikosini
Ni dakika 90 za nguvu, dakika 90 za jasho na damu kusaka ushindi kwenda fainali...!