Yanga imepania kwenda fainali ASFC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 May 2022
Yanga imepania kwenda fainali ASFC

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wamejiandaa vyema kuelekea mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba

Nabi amesema wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa katika mchezo huo kwani wanakutana na timu ambayo inaweza kutumia makosa kuwaadhibu

"Tumejiandaa kikamilifu kwa ajili mchezo huu. Tutacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha tunapata matokeo yatakayotupeleka hatua ya fainali"

Nabi amesema nidhamu ya wachezaji ndio iliyowapa mafanikio waliyopata mpaka sasa msimu huu, ni muhimu kwa wachezaji kuzingatia

"Nilisema wakati nafika hapa Tanzania mara ya kwanza, hakuna kitu muhimu kama nidhamu kwa wachezaji na hata sisi makocha na wasaidizi wangu wengine"

"Kuna staa mmoja tu kwenye klabu hii ambaye ni Yanga na sio mimi au mwingine. Tunaendelea na maandalizi, kitu muhimu ambacho nimewaambia wachezaji ni kujituma kuanzia kwenye maandalizi mpaka kwenye mechi, tumekuwa tunashinda kwa nidhamu yetu kama timu na sio nguvu ya mtu mmoja," alisema Nabi

Nabi amesema wachezaji Dickson Ambundo na Saido Ntibazonkiza ni mara yao ya kwanza kufanya makosa, wameadhibiwa lakini bado ni wachezaji wa Yanga

Nae kiungo Deus Kaseke akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, amesema morali yao iko juu akiwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao siku ya Jumamosi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
32m ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
50m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
56m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’