Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli ametaja sababu ya kikosi chao kuweka kambi yake mkoani Shinyanga kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao utapigwa Jumamosi, May 28 katika uwanja wa CCM Kirumba
Bumbuli amesema Yanga ililazimika kuondoka jijini Mwanza baada ya kukosa viwanja vizuri vya kufanyia mazoezi kutokana na vile vilivyopo kuchukuliwa vyote na Simba
Bumbuli amesema wameridhika na uamuzi wa kwenda Shinyanga kwani umekuwa na faida kwao kwani wamepata utulivu na kuwasaidia kuweka umakini katika maandalizi ya mchezo
"Tulikwenda Shinyanga kwa sababu Simba wali-book viwanja vyote vilikuwa vimeshachukuliwa tulikwenda Nyamagana, Butimba na hata Gwambina kote tukaambiwa wenzetu wameshaulizia"
"Kama unavyojua tamaduni za hizi timu mbili ukishakwenda mahali ukasikia tu mwenzako ameulizia ama alikuwepo basi hiyo sehemu haukai. Hili halitutoi mchezoni limetupa nafasi nzuri ya utulivu na ku-concetrate na mazoezi, vile vile kwenda Shinyanga ni plan zetu tutarejea Mwanza siku ya mechi (Jumamosi)"
"Maandalizi yanakwenda vizuri hadi sasa kikosi hakina majeruhi dhamira yetu ni kufika fainali. CCM Kirumba ni Uwanja wa nyumbani na Mwanza ni kama nyumbani tumekuja kwenye Uwanja ambao tuna rekodi nzuri nao"
"Wana Yanga waje wakijua sherehe zetu zinaanza Jumamosi tunaingia uwanjani kwa malengo ya kuitoa Simba tunafahamu wamewekeza nguvu hapa"
"Tunawaheshimu wana kikosi kizuri ni bingwa mtetezi wa kombe hili na kwa kuzingatia tumewanyang'anya kombe utakuwa mchezo mgumu, tumejiandaa kwa ajili ya kushinda lakini hatuendi na matokeo mfukoni," alisema Bumbuli