Hatutawadharau Biashara United - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 May 2022
Hatutawadharau Biashara United - Nabi

Licha ya kuwa katika nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wataikabili Biashara United kwa tahadhari kubwa katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba Jumatatu

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Nabi amesema Biashara United wana kikosi kizuri na pengine hawakustahili kuwa katika nafasi waliyopo

Hata hivyo amesema Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na malengo ya kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa

"Ni mchezo muhimu sana kwetu kupata ushindi. Hata hivyo tunakwenda kukutana na timu ngumu ya Biashara United hivyo tunapaswa kuingia kwa tahadhari kubwa"

"Mechi mbili zilizopita dhidi yao zilikuwa na ushindani hivyo tunatarajia mchezo wa Jumatatu utakuwa hivyo," alisema Nabi

Nabi amesema wako karibu kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa, alama tatu zitazidi kuwaweka karibu na ubingwa huo

Amesema hawataingia katika mchezo huo wakiwa na mawazo ya sherehe za ubingwa, kama itatokea ushindi utawapa ubingwa basi litakuwa jambo zuri kwao lakini kama itakuwa tofauti basi wataendelea na mkakati wao katika mchezo utakaofuata

Leo Geita Gold inachuana na Simba katika mchezo unaopiwa uwanja wa CCM Kirumba. Kama Geita Gold itashinda mchezo huo, Yanga inaweza kutwaa ubingwa kesho iwapo itapata ushindi dhidi ya Biashara United

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’