Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza hapo jana umewafanya Wananchi wafikishe alama 63 katika michezo 25 waliyocheza mpaka sasa
Yanga imefunga mabao 41 na kuruhusu mabao sita tu kutikisa nyavu zake, tofauti ya mabao ni 35
Simba inayoshika nafasi ya pili imekusanya alama 50 huku ikifunga mabao 32 na kuruhusu mabao 11, tofauti ya mabao ni 21
Kwa maana Wananchi wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 13 na mabao 14 dhidi ya Simba
Yanga haijaruhusu kufungwa bao katika michezo mitano iliyopita mlinda lango Djigui Diarra akikusanya jumla ya cleansheet 15 wakati Aishi Manula wa Simba ana cleensheet 11 tu
Wananchi wanahitaji alama sita tu kuwa mabingwa, pengine itakapofika Jumatatu baada ya mchezo wao dhidi ya Biashara United zitabaki alama tatu tu
Mambo yanaweza kuwa mazuri mapema zaidi kama Geita Gold watapata ushindi dhidi ya Simba hapo kesho na Yanga kuifunga Biashara United, hesabu za ubingwa zitatimia!