Leo majira ya saa moja usiku vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya Kwanza katika mchezo wa ligi, raundi ya 25
Ni mchezo muhimu kwa Yanga katika mpango wao wa kutwaa ubingwa wakihitaji alama tisa kukamilisha jambo lao
Kocha Mkuu wa Yanga Nasredine Nabi amesema wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo huo huku akibainisha kuwa hawatawadharau wapinzani wao
Ushindi kwa Yanga utawafanya wafikishe alama 63 na kuendelea kuwa karibu zaidi na ubingwa
Aidha kama Simba watakosa ushindi dhidi ya Geita Gold Jumapili, ushindi kwa Yanga leo utawafanya wawe na nafasi ya kutangaza ubingwa katika mchezo ujao dhidi ya Biashara United ambao utapigwa uwanja wa CCM Kirumba siku ya Jumatatu
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani leo akieleza kutakuwa na jambo kubwa litatangazwa hapo uwanjani