Winga Jesus Moloko alikuwa na kiwango bora sana kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, Moloko alihusika katika mabao yote mawili akitoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na Dickson Ambundo na baadae kumtengea pasi murua Zawadi Mauya ambaye shuti lake lilimshinda mlinda lango wa Dodoma Jiji na kujikuta akiutumbukiza mpira kimiani
Ulikuwa mchezo wa kwanza Moloko ameonyesha kiwago bora tangu aliporejea kutoka kwenye majeraha
Msimu huu Moloko amefunga mabao matatu lakini amekuwa akikosolewa kuwa ufanisi wake umekuwa mdogo mbele ya lango
Mwenyewe anasema zipo nyakati ngumu ambazo kila mchezaji hupitia lakini baadae mambo huwa sawa
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameonyesha imani kubwa kwake, kwa hakika katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hakumuangusha