Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea kwenye dimba la Taifa Februari 06 kuivaa Njombe Mji kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 17.
Mchezo huo utapigwa siku tatu baada ya Yanga kuivaa Lipuli FC mkoani Iringa.
Ratiba hiyo itaendelea kubaki hivyo baada shirikisho la soka nchini (TFF) kuigomea Simba iliyoomba mchezo wake dhidi ya Azam FC uliopangwa kupigwa Februari 07 uahirishwe ili kuipa nafasi ya kujiandaa na michuano ya Kimataifa.
TFF imekwepa lawama ya 'upendeleo' kwani kama ingekubali ombi la Simba basi ingelazimika kuahirisha mchezo wa Yanga dhidi ya Njombe Mji kwa kuwa nao umepangwa Februari 06 huku Yanga ikikabiliwa na mchezo wa awali ligi ya mabingwa dhidi St Louis Februari 10.
Hata hivyo TFF imeahirisha mchezo wa ugenini wa Simba dhidi ya Mwadui FC ambao ulipangwa kupigwa Februari 14.
Baada ya kucheza na St Louis, Februari 10, Yanga itashuka tena dimbani Februari 14 kuivaa Majimaji kwenye uwanja wa Taifa.

ADVERTISE HERE