Kiungo Salum Abubakar 'Sureboy' atakuwa na nafasi ya kusaidia Yanga katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Simba May 28
Sureboy ameonyesha kiwango bora katika michezo iliyopita na kubwa zaidi ameonyesha kumudu mazingira ya viwanja vyenye changamoto
Juzi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji, Sureboy alikuwa anatereza kama kambale katika uwanja wa Jamhuri
Akishirikiana vyema na Zawadi Mauya, waliweza kuwavuruga kabisa Dodoma Jiji katika eneo la kiungo na kuifanya Yanga iwe na umiliki kwa mpira kwa asilimia 70 licha ya uwanja kutokuwa bora
Hakuna shaka Sureboy atakuwa silaha muhimu ya Kocha Nasreddine Nabi katika mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa May 28 katika uwanja wa CCM Kirumba
Utakuwa mchezo wa nne kuzikutanisha Yanga na Simba msimu huu, Yanga ikishinda mchezo mmoja (Ngao ya Jamii) huku mechi mbili za ligi kuu zikimalizika kwa suluhu ya bila kufungana