Msemaji wa Yanga Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi kuu unaofuata
Yanga itakuwa mwenyeji wa Mbeya Kwanza katika mchezo utakaopigwa Ijumaa, May 20 2022, mchezo huo ukirudishwa nyuma kwa siku moja
Manara amesema wako katika nafasi nzuri ya kushinda ubingwa lakini hawajashinda, sapoti ya mashabiki katika michezo hii ya mwishoni ni muhimu kuwapa motisha wachezaji katika kusaka matokeo
"Haiwezekani hawa wanaume wana pointi 60, wanakuja kucheza nyumbani, hawajapoteza hata mchezo mmoja, wanaongoza kwa kila takwimu halafu wewe shabiki wa Yanga huji uwanjani, halafu unajiita Mwananchi! HAIWEZEKANI," alisema Manara
ADVERTISE HERE