Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Dodoma Jiji ni matokeo muhimu waliyoyahitaji
Mayele amesema halikuwa jambo zuri kwa timu kubwa kama Yanga kukosa ushindi katika michezo mitatu mfululizo, leo waliingia uwanjani wakiwa na dhamira ya kushinda
Aidha Mayele amesema yeye ni mchezaji wa Yanga anapofunga anaisaidia timu kutimiza malengo lakini pia hata anapofunga mchezaji mwengine, inayonufaika ni Yanga
"Tunamshukuru mwenye ez mungu kwa ushindi huu. Ilikuwa mbaya kwa timu kubwa kama Yanga kucheza michezo mitatu bila ya kushinda. Tumepata ushindi, tunasonga mbele mchezo unaofuata"
"Muhimu ilikuwa ushindi, Yanga kwanza halafu hesabu ya mabao baadae. Naamini tu nitafunga wakati wangu utafika, ni kawaida kwa mshambuliaji kupitia kipindi kama hiki," alisema Mayele
Mabao ya Dickson Ambundo na Zawadi Mauya yaliihakikishia Yanga alama tatu muhimu
Yanga ilikuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi mnono zaidi, Ambundo na Nkane wakiporeza nafasi adimu
Wakati safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji ikiwa makini kumkaba Mayele, mabao yakafungwa na wengineee!