Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons, kikosi cha Yanga kiliingia kambini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa Jumapili, May 15 katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma
Huu ni mchezo ambao Yanga inapaswa kuukabili kimkakati zaidi kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu
Matokeo ya ushindi yatarejesha ari ya wachezaji kuelekea michezo sita itakayokuwa imesalia kukamilisha msimu huu
Huu utakuwa mchezo wa fainali kwelikweli, ni kufa au kupona
Bado hesabu za Yanga kuelekea ubingwa wa 28 ziko salama lakini muhimu ni kuhakikisha matokeo ya ushindi yanapatikana katika michezo yote iliyobaki
Mkakati uwe kutwaa ubingwa haraka iwezakanavyo ili kukamilisha mechi mwisho pasipo kuwa presha yoyote
ADVERTISE HERE